Bunge lawapa mzigo walipa ushuru ili kuwalipa pensheni wabunge wa zamani

Bunge
Bunge
Walipa ushuru watalazimika kubeba mzigo zaidi  ili kufadhili pensheni ambayo serikali inataka kuwalipa wabnge wa zamani mbao walihudumu kati ya mwaka wa 1984 na 2001

Bunge litapiga kura leo kufanyia marekebisho sheria ya malipo ya uzeeni ili kuwapa wabunge hao wa zamani  pensheni watakayolipwa kila mwezi maisha yao yote .

Marekebisho hayo yaliofanywa kwa sheria ya  malipo ya  uzeeni kwa wabunge  yatapitishwa kwa urahisi bungeni .pensheni hiyo ya kila mwezi  itaongezwa kutoka shiingi 2000 kwa sasa hadi shilingi 125,000 kila mwezi .

Malipo ya fedha hizo huenda yakarejeshwa nyuma hadi julai mwaka wa 2010  hatua ambayo  huenda ikailazimu serikali kutoa mamilioni ya pesa kutekeleza pensheni hiyo .

Iwapo rais Uhuru Kenyatta ataidhinisha msswada huo kuwa sheria wabunge 290 huenda wakaanza kulipwa kiasi cha chini ya shilingi 100,000 kama pensheni kila mwezi

Ofisi ya bajeti bungeni  imeashiria kwamba serikali huenda ikawalipa wabunge hao wa zamani shilingi milioni 15.1 kila mwezi .