BURIANI BRYANT: Picha za baada ya  ajali ya ndege iliyomuua Kobe Bryant,bintiye na watu wengine 7

Picha zilizopigwa baada ya ajali ya ndege ya helikopta iliyosababisha kifo cha staa wa zamani wa NBA Kobe Bryant  zimetolewa. Ndege ya Bryant ilianguka  katika bonde kutoka umbali wa futi 1000 baada ya rubani  kujaribu kupaa juu zaidi ili kuepuka ukungu siku ya jumapili.

Picha zilizopigwa baada ya ndege hiyo kuanguka zinaonyesha mabaki ya ndege hiyo yakiteketea. Shahidi aliyezipiga picha hizo amesema aliona  vifaa vya  helikopta vikitapakaa kila mahali  kisha baadaye mlipuko mkubwa uliofuatwa na moto.

Rubani  Ara Zobayan alikuwa ametaka kupewa idhini na kukubaliwa kupaa katika hali iliyokuwa na ukungu mwingi  akiwa juu kwa umbali wa futi 1400 muda mfupi kabla ya ajali hiyo kutokea. Wachunguzi wamesema hapakuwa na kifaa maalum cha kunakili safari ya ndege hiyo bali  kipakatilishi kidogo kilichokuwa kikitumiwa kuonyesha mkondo wa safari ya ndege hiyo. Maafisa wa usalama wanatumia farasi kushika doria katika eneo la mkasa la Calabasas, California ili kuwazuia waporaji kufika huko .