Willy Paul adai kumripoti kwa polisi Shakilla kwa kuingia nyumbani kwake bila idhini

Muhtasari

 • Willy Paul apelekea kukamatwa kwa mwanasosholaiti Shakilla

 • Shakilla aliingia nyumbani kwa msanii huyo bila idhini yake.

 • Mwanasosholaiti huyo aliingia nyumbani mwa Paul usiku wa manane

Willy paul
Willy Paul Willy paul
Image: Hisani

Mwanamuziki Willy Paul amewashangaza wengi wakiwemo wasanii wenzake baada ya kukiri kwamba yeye ndiye sababu ya Shakilla kukamatwa, hii ni baada ya mwanasosholaiti huyo chipukizi kuingia nyumbani kwake usiku wa manane bila idhini yake.

Kulingana na Willy Paul Shakilla alifaulu kuingia nyumbani kwake baada ya kuruka juu ya lango kuu. Kupitia mitandao ya kijamii Paul alisema kuwa alimripoti Shakilla katika kituo cha polisi na hatimaye akatiwa mbaroni.

Alisema kwamba kwa muda huo wote hakujua kuwa alikuwa ni Shakilla hadi pale walipokutana ana kwa ana.

 
 

Huku akizungumzia tukio hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Poze alikuwa na haya ya kusimulia;

"Nataka kuzungumzia jambo ambalo lilitokea jana nyumbani kwangu saa sita za usiku wa manane. Mabawabu wa ngu waligundua kuwa kuna mwanamke ambaye alikuwa katika lango kuu na ambaye alikuwa anajilazimisha kuingia nyumbani kwangu...

Walinifahamisha haraka nilipoenda kufahamu kuwa ni nani nilipata ni 'Famous shakilla' niliripoti kwa polisi  na alikamatwa kwa kuingia kwangu bila idhini." Aliandika Willy Paul.

Pia msanii huyo alisema kuwa Shakilla aliwataja baadhi ya watu ambao anafanya nao kazi yake.

"Nilipeana ushahidi wa kamera za CCTV, na alitaja baadhi ya majina ya watu ambao anafanya kazi nao kwa maafisa wa polisi kwa uchunguzi zaidi...Niwekeni kwa maombi yenu pamoja na familia yangu, siko salama kwa sasa." Paul Aliandika.

(Mhariri Davis Ojiambo)