'Mungu ni mwema,' Ghost azungumza baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabara

Muhtasari
  • Ghost Mulee azungumza na kuwashukuru waliomtakia afueni ya haraka
  • Alipelekwa katika hospitali ya Agha Khan, ambapi alipokea matibabu
ghost mulee

Mtangazaji wa Radiojambo Jacob Ghost Mulee baada ya kuhusika katika ajali asubuhi ya Ijumaa hatimaye ameweza kuzungumza na kuwashukuru wote ambao walimtakia afueni ya haraka.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagramaalikuwa na haya ya kunakili;

"Mungu ni mwema, nimefanyiwa vipimo baada ya ajali ya asubuhi ya leo na nimemaliziwa na daktari katika hospitali ya Aga Khan 

 

nachukua fursa hii kumshukuru kila mmoja wenu ambaye alinitakia afueni ya haraka, ilikuwa jambo la haraka Mungu ni mwema kila wakati." Aliandika Ghost.

Ujumbe wake ulipokelewa vyema na mashabiki huku wengi wakizidi kumtakia afueni ya haraka.

Ghost alikuwa anaelekea kazini alipopata ajali hiyo, na kupelekwa katika hospitali hiyo na mtangazaji mwenzake Jalang'o ambaye alieleza kuhusu ajali hiyo.

Mtangazaji huyo aligongwa na matatu ambapo iligonga upande wa dereva, na gari lake kupelekwa katika kituo cha polisi cha Spring Valley.