'Nilikuwa napata shilingi 93 kila siku,' Diamond azungumzia kazi aliyokuwa anafanya kabla ya kufahamika

Muhtasari
  • Nilikuwa nauza Mitumba kwa maana kila mtu alikuwa ananitegemea nyumbani
  • Nilikuwa napata mapato ya shillingi 93 kwa siku Diamond afichua
diamond-platnumz
diamond-platnumz

Staa wa bongo Diamond Platnumz alikuwa hustler wa kawaida kabla ya kuanza usanii wake enzi zile, huku akiwa kwenye mahojiano Diamond alisema kuwa alikuwa anauza mitumba na kupata shillingi 93 pesa taslimu za kenya.

"Nilikuwa nauza mitumba, kutoka asubuhi saa mbili hadi saa kumi jioni bila kupumzika." Alisema msanii huyo.

Huku akizungumzia mapato yake alisema ya kwamba alikuwa anapata shillingi 2000 pesa taslimu za Tanzania huku kila mtu katika familia akimtazama.

 

"Nilikuwa napaya TSH 2000(Ksh.93)."

Awali akiwa katika mahojiano Diamond alisema kwamba alikuwa mfanyakazi katika kituo cha petroli na pia mpiga picha.

Kwa kweli hawakukosea waliposema ya kwamba aijuaye kesho ni Mungu kwa maana nyakati zile kama msanii huyo angeulizwa kama angejulikana afrika mashariki nzima na duniani kote hangeamini wala kujibu swali hilo