'Mjinga fulani,'Mwanamke aliyeonekana na Omar Lali amsuta vikali mwanablogu Cyprian Nyakundi

Muhtasari
  • Mwanamke aliyeonekana na Omar lali akana madai kuwa ni mpenziye
  • Hii ni baada ya mwanablogu huyo kupakia picha ya wawili hao na kudainkwamba ni wapenzi

Miyandao ya kijamii ilijaa hisia tofauti kutoka kwa wanamitandao baada ya picha yake aliyekuwa mpenzi wake Tecra Muigai Omar Lali akiwa na mwanamke aliyefahamika kama Koko Kamillah kuenea sana.

Wawili hao kaika picha hiyo walionekana wakiwa wamekaa chini huku wanamitandao wengi wakidai kwamba Omar amepata mpenzi wake wa maisha.

Ni picha ambayo ilipakiwa na mwanablogu Cyprian Nyakundi, huku wengi wakisema kwamba ni wapenzi.

 

Baada ya Koko kuona picha hiyo na kuambiwa kwamba anavuma mitandaoni kwa mabaya, hatimaye ameamua kuongea na kusema kwamba yey si mpenzi wake Omar bali ni rafiki wake wa kitambo.

Pia mwanamke huyo alisuta vikali Nyakundi kwa kueneza habari mbaya kumhusu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Koko alikuwa na haya ya kusema kuhusu picha hiyo.

"Kwa hivyo niliamka hii leo asubuhi na kupatana na jumbe nyingi kwenye ukurasa wangu wa instagram na hata WhatsApp zikiniambia kwamba navuma kwa sababi zote mbaya

Mjinga fulani @Cyprian Nyakundi alichukua picha yangu nikiwa na rafiki yangu wa kitambo  Omar Lali na kupakia picha yangu nje ya manukuu ya muktadha

Lakini sasa nafurahia ujinga huo." Aliandika Koko.

 

Licha ya yake kujibu madai ya kwamba yeye si mpenzi wake Omar wengi wamesalia na maswali chungu nzima yenye hayana majibu.