Poleni sana! Omar Lali akana madai kwamba ni mpenziwe Koko

Muhtasari
  • Omar Lali awakashifu vikali waliosema kwamba ni mpenzi wake Koko Kamilah
  • Omar alisema kwamba hana mpenzi na wakati haujafika wake wa kuwa na mpenzi

Omar Lali aliyekuwa mpenzi wake mwendazake Tecra Muigai atimaye amezungumza na kutupilia mbali madai kwamba ni mpenzi wa mwanamke anayefahamika akama Koko Kamilah.

Hii ni baada ya picha ya wawili hao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na wanamitandao kudai kwamba wawili hao ni wapenzi.

Kupitia kwa video aliokana madai hayo pia Omar alisema kwamba watu wawache kueneza habari zizsizo za kweli.

 

"Nimemjua Koko kwa miaka mingi , ni rafiki yangu na wala si mpenzi wangu, sina mpenzi kwa hivyo vyovyote vinaandikwa kwenye vyombo vya habarina magazetti, poleni sana wakati bado haujafika

Na kama wakati huo upo nyinyi watu mtajua kwa maana niko hapa, ninaishi na bado mimi ni binadamu

Omar Lali
Omar Lali

Kwa hivyo usichukue faida kwa watu na uandike vitu vya kijinga, kwenye twiter,facebook,ama kwenye magazetti

Tafadhali kuweni na maisha, kama hauna chochote cha kufanya kuja Lamu tukupeleke ukavue." Omar Alisema.

Usemi wake Omar unajiri saa chache baada ya Koko pia kukana madai hayo na kusema kwamba Omar ni rafiki wake wa ktambo.

Pia alimsuta vikali mwanablogu Cyprian Nyakundi kwa kuchukua picha hiyo na kusema kwamba wawili hao ni wapenzi.

"Kwa hivyo niliamka hii leo asubuhi na kupatana na jumbe nyingi kwenye ukurasa wangu wa instagram na hata WhatsApp zikiniambia kwamba navuma kwa sababi zote mbaya

 

Mjinga fulani @Cyprian Nyakundi alichukua picha yangu nikiwa na rafiki yangu wa kitambo Omar Lali na kupakia picha yangu nje ya manukuu ya muktadha

Lakini sasa nafurahia ujinga huo." Aliandika Koko.