'Salum Iddi Nyange ndiye babake Diamond' - Mama Dangote

Habari kubwa zaidi kutokea Tanzania ni kuwa Mama Dangote ametangaza kuwa mzee Abdul sio babake mzazi Diamond Platnumz ile yeye ni baba mlezi.

Akizungumza moja kwa moja na stesheni ya Wasafi FM , mama Dangote alisema kuwa babake Diamond ni marehemu Salum Iddi Nyange.

Mama Dangote pia alifichua kuwa  mzee Abdul alimpata akiwa na mimba.

Habari hizi za kushangaza zitafikisha kikomo, mvutano uliokuwa kwamba Abdul ametengwa na mwanawe Diamond.

Akizungumza na kituo cha Bongo 5, mzee Abdul anasema kuwa baada ya kupokea habari hizo, anapaswa kupongezwa ila sio kupewa pole.

Mama Dangote ashasema kuwa Diamond sio mtoto wangu, mhusika ashasema sio mtoto wangu kwa hivyo sio mtoto wangu.

Babake kafa tena kaoneshwa kaburi la babake na akaambiwa asitumie jina langu baas, nadhani hayo yatosha kwa leo." Alisema mzee Abdul.

Aliongeza,

Namuombea (Diamond) maisha mazuri ataenda kuoneshwa kaburi la babake akate mawasiliano na mimi, mimi sio mzee wake asitumie jina langu.

Mzee Abdul asema kuwa anahisi ni kama ameutua mzigo kwani jambo hili limemsumbua mawazo kwa mda mrefu huku akisema anafaa kupewa pongezi ila sio pole.

Hata hivyo, mzee Abdul alikuwa na ombi moja kwa wanaTanzania;

"Mimi naomba wananchi wasinipige tena picha yaani wanaona kumbe nikibeba viatu ni kazi zangu. Sasa hivi nafanya biashara ya kuuza midundo."