- Carol ambaye alimaliza kama mshindi ili kuwa ‘mke’ wa Omondi amekana kuwa alishiriki mapenzi na Eric Omondi wakati wakiwa katika ‘ honey moon’ huko pwani
- Watu wengi hawaamini kwamba hakuna kilihofanyika katika siku moja au mbili ambazo Omondi na Carol walikuwa pwani
Waimbaji wa kundi la BandBeca Carol na Becky waligonga vichwa vya Habari kwa kushiriki katika kipindi cha maigizi cha Eric Omondi ,Wife material
Carol ambaye alimaliza kama mshindi ili kuwa ‘mke’ wa Omondi amekana kuwa alishiriki mapenzi na Eric Omondi wakati wakiwa katika ‘ honey moon’ huko pwani
Watu wengi hawaamini kwamba hakuna kilihofanyika katika siku moja au mbili ambazo Omondi na Carol walikuwa pwani . Carol akizungumza katika kipindi cha Ilikuaje cha Maqssawe Japani katika radio Jambo hata hivyo amesema yote yalikuwa maigizo na kwamba alihusika katika kipindi hicho ili kutangaza album yao ya muziki .
“ Hatukulala katika chumba kimoja ,iwapo hicho ndicho unachouliza .kila mtu alikuwa katika chumba chake
Sababu ya watu wengi kutoamini kauli ya Carol ni kwamba palitokea picha nyingi ambazo walipiga katika sehemu mbali mbali zikiwemo katika bafu … huku katika picha nyingine wakionekana kukumbatiana na wakipapasana .
“ Hakuna kilichofanyika na iwapo ningepata mimba ya ERIC BASI NITAIHIFADHI ..LAKINI SASA HAKUNA WATOTO .