Kifo chake Papa Shirandula kilinipa pigo kubwa-Muigizaji Omosh aomboleza

Muhtasari
  • Omosh aeleza jinsi alivyopata pigo baada ya kifo cha muigizaji mwenzake Papa Shirandula
Joseph Kinuthia
Image: Ivy Muthoni

Muigizaji wa kipindi cha Tahidi High Joseph Kinuthia almaarufu Omosh akiwa kenye mahojiano na Radiojambo alizungumzia jinsi alivyopatwa na pigo kubwa baada ya kusikia kifo chake Papa Shirandula.

Papa Shirandula aliaga dunia mwaka jana kwa njia tatanishi.

Omosh alisema kwamba alikuwa kwenye kipindi cha Tahidi high kwa muda wa zaidi wa miaka kumi.

 

"Kifo chake Papa kiliku pigo kubwa kwangu,tulipatana wakati alikuwa kwenye kipindi cha maktano junction nilikuwa natembea huko, nilikuwa muigizaji tu wale wa kujaza filamu yaani wale wa nyuma

Papa aliniita na kuniambia kuwa anaona kitu ndani yangu, kutoka hapo tulikuwa marafiki yaani damu zetu zilikubaliana

Kutoka hapo tulipatana tena Tahidi high." Alizungumza Omosh.

Huku akizuungumzia kazi ya uigizaji Omosha alisema kuwa,

"Ukieza jua kiasi ambacho tulikuwa tunapewa, kila uigizaji tulikuwa tunalipwa shillingi elfu 18,000 na labda uigizaji wako ni mara mbili kwa mwezi

Kwa hivyo lazima utafute kazi nyingine ya kufanya ili utimize mahitaji yako, lakini wakati huo nilikuwa mlevi nakumbuka nilipoteza miaka 15 kwa pombe

Natamani ningekuwa na mtu wa kunishauri,unapata jina lako ni kubwa na unafahamika sana lakini kwenye mifuko yako hamna kitu, pia hatulipwi marudia mbayo yanafanyika kwenye runinga."

Tazama video ya mahojiano hayo hapa;

Radio Jambo Kenya | Ongea Usikike | Ni kituo nambari moja Kenya kwa matangazo ya kiswahili. Vipindi vyake vina jumuisha Spoti,Mijadala moto moto na muziki wa Kiafrika #RadioJamboKenya Subscribe to RadioJambo Youtube - https://bit.ly/39wwc6u Mitandao ya Kijamii Instagram - https://rb.gy/e154d1 Facebook - https://rb.gy/09d1b9 Twitter - https://rb.gy/e23220