Watu mashuhuri ambao walijutia kubugia vileo sana katika maisha yao

Muhtasari
  • Oorodha ya watu mashuhuri waliojutia kubugia vileo,Kulingana na uchunguzi wangu watu wengi mashuhuri huwa wanaingia katika pombe bila ya kujua maisha yao ya kesho
ethanol
ethanol

Pombe si jambo ambalo mke wa mtu au mume au mpenzi wa mtu angetaka mwenzake anywe kwa muda.

Kuna wale wanasema kwamba pombe si mbaya, ndio pombe kidogo sio mbaya pombe ambayo unaelewa wewe ni nani na unaenda wapi hiyo si mbaya.

Lakini kuna baadhii ya watu ambao hukunywa pombe wanakosa kujielewa na hata kusahau majina yao. 

 

Kuna wale ambao hujipa kwenye mitaro wakiwa wamelala huko kwa maana walibugia pombe bila ya kujali.

Tume wasikia na kuwaona watu mashuhuri wakikiri kwamba katika maisha yao ya awali walibugia vileo sana na kisha maisha yao yanasambaratika.

Kulingana na uchunguzi wangu watu wengi mashuhuri huwa wanaingia katika pombe bila ya kujua maisha yao ya kesho.

Hutapata wabugia vileo wengi hawawekezi pesa zozote wala hawana akiba ya kutegemea.

Wengi husema kwamba pombe hutoa msongo wa mawazo ambapo, ni shida ambayo mtu huwa anajiongezea katika maisha yake.

Katika makala haya tunazingatia watu mashuhuri ambao walikiri na kujutia kubugia vileo sana.

Hii hapa orodha ya baadhi ya watu hao;

 

1.Joseph Kinuthia(Omosh)

Alikuwa muigizaji wa kipindi cha Tahidi High, ambaye mwezi uliopita alijitokeza na kufichua mambo na changamoto ambazo amekuwa akipitia na hata kuwa ma madeni mengi.

Joseph Kinuthia
Image: Ivy Muthoni

Akiwa kwenye mahojiano na radiojambo alisema kwamba alifunzwa kubugia vileo na marafiki, ambapo baadaye alikuwa mwenyeji wa vileo.

2.Jackline Nyaminde(Wilbroda)

Nyaminde alifahamika sana akiwa kwenye kipindi cha papa shirandula ambapo alikuwa anaigiza kwa jina la Wilbroda.

Akiwa kwenye mahojiano muigizaji huyo alifichua kwamba alibugia pombe sana huku maisha yake yakirudi na nyuma.

3.Njoro

Ni mchekeshaji wa kipindi cha Churchill show na ambaye aliingia katika ulevu huku mwishowe akija kuokolewa na mcheshi mwenzake na hata kumpeleka shule ya mafunzo yaani Reharb.

Njoro
Njoro

Baada ya kutoka katika mafunzo hayo alibadilika na hata kuendelea na maisha yake na kupata kai