(+video) Msinitumie jumbe mkiniuliza kuhusu shoo ya 'wife material' siko hapo-Eddie Butita

Muhtasari
  • Mchekeshaji Eddie Butita ajitenga na kipindi chake Eric Omondi

Mchekeshaji Eddie Butita amejitenga na madai kwamba yumo katika shoo ya Eric Omondi ya 'Wife Material'.

Haya yanajiri baada ya Eric Kutiwa mbaroni, huku Butita akipokea jumbe kutoka kwa wanamitandao huku wakimuuliza hiyo ni shoo gani ambayo wametengeneza na Eric.

Huku akipakia video kwenye ukurasa wake wa instagram Eddie alisema kwamba hayumo kwenye shoo hiyo, na alimuonya Eric wapange kipindi chake lakini hakusikia.

"Baada ya Eric kukamatwa nimekuwa nikipokea jumbe nyingi mimi nisitumiwe jumbe wala maswali yeyote kwani siyuko katika shoo ya 'Wife material' nimejitenga na kipindi hicho

Kipindi hicho hakijaandikwa,nilimuonya eric tupnge kipindi hicho lakini hakunisikia ona sasa alikamatwa,ata siyuko Nairobi, niko Kisumu nikifanya miradi yangu ingine

Shoo inaitaji mpangilio na mwelekeo," Alisema Butita.

Hii hapa video hiyo;