Ikiwa hauko tayari kuwa katika uhusiano na mwanamume usichukue zawadi-Loise Kim

Muhtasari
  • Loise Kim awashauri wanawake kuhusu uhusiano wa kimapenzi
Loise KIm
Image: Instagram

Msanii wa nyimbo za kikuyu Loise Kim kwa mara tena amewashauri wanawake kuhusu uhusiano wa kimapenzi.

Awali tumeona habari kuhusu jinsi wanawake waaga dunia kutokana na uhusiano wa kimapenzi.

Loise kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwashauri wanawake wasijaribu kuchukua zawadi za wanaume kama hawayuko tayari kuwa katika uhusiano.

 

Pia alisema kwamba wanaume wametumia mbinu tofauti ili waweze kupendwa na wanawake, bila ya kujua wala kufahamu kama wanawapenda.

"Kuwekeza hisia zako, fedha, wakati wako kwa mtu asiyestahili kunakufanya uwe duni. Wanawake ikiwa haujawa tayari kwa uhusiano usichukue zawadi

Wanaume, wengi wenu mmetumia mbinu ya kupeana ili kuvutia na kupendwa, hakikisheni juu ya Uhusiano wa kujitolea na muwache kuruka ruka, ambapo uwekezaji wako unapata sawa. Ndio inaumiza, lakini ....... Mwishowe, ukiwachwa achika," Loise Aliandika.

Wengi hukosea kwenye safari ya mapenzi na kumpata umemuoa mtu ambaye sio wa ubavu wako na kusumbuana milele.