'....niondolee ujinga na upuzi kutoka moyoni mwangu,'Size 8 aomba haya

Muhtasari
  • Safrai ya wokovu ya msanii wa nyimbo za injili Size 8 inafahamika vyema na mashabiki wake na wanamitandao
  • KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alimisi Mungu amuondolee ujinga na upuzi kutoka moyon mwake ili aweze kumtumikia awezavyo
Size 8
Image: maktaba

Safrai ya wokovu ya msanii wa nyimbo za injili Size 8 inafahamika vyema na mashabiki wake na wanamitandao.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alimisi Mungu amuondolee ujinga na upuzi kutoka moyon mwake ili aweze kumtumikia awezavyo.

Pia alimuomba Mungu ampe hekima ya neno lake na kutofauisha mazuri na mbaya ya ulimwengu.

Kupitia kwa ujumbe wake mwingine alieleza mashabiki wake kile roho mtakatifu amemfunza kuhusu maisha.

"Baba Mungu ninaomba kwa jina la Yesu niondole ujinga na upuzi kutoka moyoni mwangu na akili yangu ili niweze kuzingatia yote niliyo nayo kukuhudumia kwa muda ni mfupi na kama Yesu alisema

"Maadamu ni mchana, lazima tufanye kazi ya yeye aliyenituma. Usiku unakuja, ambao hakuna mtu awezaye kufanya kazi "

Woi naomba mungu wangu nipe Hekima kutoka kwako, kusema ndio kwako na hapana kwa ulimwengu hivi karibuni na hivi karibuni wote tutatoa hesabu mbele yako juu ya jinsi tulivyoishi maisha yetu hapa duniani !!! Yote ninayotaka wewe kuniambia siku hiyo ni Mtumishi mwema na Mwaminifu Kwa jina la Yesu amina," Aliandika Size 8.

Msanii huyo amekuwa akitoa kibao kimoja baada ya kingine na hata kufanya collaboo na wasanii tofauti wa nyimbo za injili huku nyimbo zake zikipendwa na mashabiki wake.