Nilimtambulisha mpango wangu wa kando kwa mke wangu-Jamaa adai

Muhtasari
  • Jamaa aeleza nini kilisababisha kumtambulisha mpango wake wa kando kwa mkewe
sad man
sad man

Je umewahi patwa na mpenzi wako na mpango wako wa kando maishani mwako kama uko naye?

Wengi hupatwa lakini wanawaficha lakini sio kwa mwanamume mmoja ambaye alishindwa la kufanya bali alifanya kumtambulisha mpango wake kwa nyumba.

Je nini kilifanyika ndiposa amtambulishe  mpango wake licha ya kufahamu mkewe ata waka moto?

"Nilimkaribisha mpango wangu wa kando kwangu, la kushangaza alikuwa anajua nina mke lakini sikuwa nimemwambia, siku moja nilimkaribisha kwangu

Alikuwa anaogopa kwani alisema kwamba tunaweza patwa na mke wangu, nilimhakikishia kwamba hatuwezi patwa," Alisema

Lakini tuseme shetani ni nini kwani ni lipi liliofuatia?

"Tukiwa tunatekeleza tendo la ndoa, kumbe nilisahau nikaacha mlango wazi, nilimsikia mke wangu akiongea nje na majirani

Nilishtuka sikuwa na lolote la kufanya, aliingia na kumpata mpango wangu wa kando, nilimtambulisha kwake

Mke wangu hakufanya lolote bali alikusanya nguo zake na akaenda, baada ya miezi tatu mpango wanu wa kando aliniacha kumbe sikujua kwamba alikuwa anataka tu pesa zangu

Sasa nataka kurudiana na mke wangu lakini amekataa kabisa turudiane, nimejua makosa yangu na nimemuomba msamaha," Alileza mwanamume huyo.

Je ukiwa mke wake unaweza mrudia, na mwanamume huyo atafanya nini ili mkewe amuamini tena?