'Mahali tumefika ni maombi tu,'Millicent Omanga awasihi wakenya kuombea nchi

Muhtasari
  • Wakenya wagadhabishwa na ujumbe wake Millicennt Omanga
  • Omanga amekuwa akikosoa mchakato wa BBI na kuunga mkono na kuendeleza kampeni za 'wheelbarrow'

Seneta mteuliwa na mfuasi sugu wa naibu rais William Ruto, Millicent Omanga kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter amewashauri wakenya waombee nchi.

Mwanasiasa huyo aliandika ujumbe huo huku akiwatakia mashabiki wake siku njema  na ibada njema siku ya Jumapili.

Omanga amekuwa akikosoa mchakato wa BBI na kuunga mkono na kuendeleza kampeni za 'wheelbarrow'.

"Kuweni na siku yenye baraka wau wangu, ombeeni nchi yetu ju mahali tumefika ni maombi tu." Aliandika Millicent.

Ni ujumbe ambao wanamitandao wametoa hisia tofauti na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

Flavia Marhlon: Especially Raila ajielewe kama ako kwa serkali ama opposition

Ray: He’s in both, question is wewe uko pande gani?

Japuonj Allen: Tumefika hapa sababu mlikataa kutekeleza majukumu yenu kama wawakilishi bunge na seneti

Y J: The last time huo wimbo wa ni "maombi tu" uliimbwa ndio tuko hapa tulipo, sasa wacha tujaribu huo uchawi !

George Kopana: We shall include our leaders in prayer too maam..Happy sunday

Ronald Barasa makokha: Wakati mwingine wanishangaza ukisema mahali tumefika ni maombi ilihali wewe na wenzako mwafaa kutushugulikia mwataka tuwaambie nini na mlipeleka tumbo zenu kujitetea

Zinirah Nanjala: Na ndio hatutaki tena kukosea kuchagua hii kitu inaitwa hustler cos their ideologies are the same.