(+Video) Bahati ajivunia albamu yake kutangazwa Marekani

Albamu yake 'Love like this' iliweza kutangazwa kwenye bango moja katika maeneo ya Times Square jijini Newyork, Marekani.

Muhtasari

•Times  Square ni ungano kuu la kibiashara, utalii na burudani jijini Newyork ambalo limezingirwa na mabango maridadi yanayotumika haswa kwa matangazo ya kitaifa.

Albamu ya Bahati, Love like this
Albamu ya Bahati, Love like this
Image: Instagram

Mwanamuziki wa nyimbo za injili na mapenzi, Kevin Bahati alizindua albamu yake mpya ‘Love like this’ siku ya Jumatatu.

Albamu hiyo yenye nyimbo kumi ilivuma sana baada ya kuachiliwa haswa wimbo ‘Pete Yangu’ ambao alishirikisha Nadia Mukami. Kwa sasa umeweza kutazamwa na zaidi ya watu 340,000 kwenye mtandao wa Youtube chini ya masaa kumi na tano baada ya kupakiwa.

Jambo la kujivunia zaidi kwa msanii yule ni kuwa albamu ile iliweza kutangazwa kwenye bango moja katika maeneo ya Times Square jijini Newyork, Marekani.

Times  Square ni ungano kuu la kibiashara, utalii na burudani jijini Newyork ambalo limezingirwa na mabango maridadi yanayotumika haswa kwa matangazo ya kitaifa.