Mlitubeba ufala! Mashabiki waambia mcheshi Jumutai na Prof Hamo

Muhtasari
  • Jemutai na Prof Hamo wazua gumzo mitandaoni
  • Tangazo hilo lilifanya watu wengi wazungumze, huku kila mtu akijaribu sana maoni yake yasikilizwe

Mcheshi wa kipindi cha churchill  Jemutai na mchekeshaji Prof Hamo wamezua gumzo mitandaoni baada ya kutangaza kwamba siku ya ijumaa watafanya shoo pamoja.

Siku ya Jumatano, wawili hao waliweka mabango kutangaza kwamba Ijumaa, 10 asubuhi, watakuwa pamoja kwenye kipindi kinachoitwa 'Bold and Candid', ambacho kitapeperushwa kwenye  YouTube.

Tangazo hilo lilifanya watu wengi wazungumze, huku kila mtu akijaribu sana maoni yake yasikilizwe.

Sehemu moja ilihisi kudanganywa na wachekeshaji hao , kufuatia mzozo wao wa umma, wiki chache zilizopita, wakati wengine walisema kwamba watu wanapaswa kujifunza kujishughulisha na biashara zao wakati wowote wanandoa wanapopambana.

Hamo akiwa kwenye mahojiano siku ya Jumatano alisisitiza kwamba yeye ni baba wa nyumba na kuongeza kuwa licha ya ugomvi wa umma, bado anachukulia uhusiano wake na Jemutai kuwa thabiti.

"Nilimwambia kuwa pia nina uchafu kwake ambao ningeweza kuchapisha kwa urahisi kwenye mitandao ya kijamii lakini nikamuuliza ni vipi hiyo itakuwa ya faida kwetu. Je! Tungeweza kukaa pamoja baada ya hapo na kuzungumza?" Alisema Hamo.

Hizi hapa hisia za mashabiki baada ya kuoona mabago hayo;

realdanieljuma: Haki nyinyi ni kama mulitubeba ufalaπŸ˜‚

hege_mathegi: Mambo ya watu hulala Duvet moja.......πŸ˜‚

j_a_p_h_i_t_h_a: Mambo ya watu wawili wamenyambiana wachana nayo...πŸ˜‚

shirley.nestor: Ile design watu wanajua kusaka doo wueh

i_am_me_she: Honestly handle your home issues privately! Kids are involved!!! Don’t come back crying again ukipata ball ya 3

gladgladu: Am just disappointed na women 😒😒 any way minding my business

edempta.m: Anakuweka karibu ndio akutoke vizuri sasa. He will be sure πŸ’― u have nowhere to complain coz hizi mitaa utaogopa matusi. U never learn na utalia tu. Atalipisha hio kumuanika ulimuanika