(+Picha) Shebesh aadhimisha kufikisha miaka 50; Wakenya mashuhuri wahudhuria hafla

Hafla ya kusherehekea siku hiyo ilihudhuriwa na watu wa tabaka mbalimbali wakiwemo watu mashuhuri nchini na viongozi wa vitengo mbalimbal

Muhtasari

•Kati ya waliohudhuria ni pamoja na gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Murang'a Sabina Wanjiru Chege,waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa, kaimu gavana wa Nairobi Anne Kananu, wabunge wa awali Linah Jebii Kilimo na Cyrus Jirongo, Karen Nyamu miongoni mwa wengine.

Waiguru, Jirongo, Shebesh na Wamalwa kwenye hafla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Shebesh
Waiguru, Jirongo, Shebesh na Wamalwa kwenye hafla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Shebesh
Image: Instagram

Aliyekuwa mwakilishi wa wanawake kaunti ya Nairobi, Rachel Shebesh aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa Ijumaa, Julai 2.

Shebesh ambaye kwa sasa anafanya kazi na wizara ya utendakazi wa umma, vijana na jinsia alisherehekea kufikisha miaka hamsini.

Kupitia mtandao wa Instagram, mwanasiasa huyo alimshukuru Mungu kwa kumpa uzima wa mwili na furaha.

"Mungu, shukran sana kwa kunipa nafasi ya kujitakia siku njema ya kuzaliwa hivi leo nikiwa na afya njema na raha. Naomba uendelee kunibariki na afya na furaha maishani. Nakushukuru Muumba wangu, unafanya kila siku ya maisha yangu kuwa ya kupendeza, ni wewe pekee waweza." Shebesh aliandika.

Hafla ya kusherehekea siku hiyo ilihudhuriwa na watu wa tabaka mbalimbali wakiwemo watu mashuhuri nchini na viongozi wa vitengo mbalimbali.

Kati ya waliohudhuria ni pamoja na gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Murang'a Sabina Wanjiru Chege,waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa, kaimu gavana wa Nairobi Anne Kananu, wabunge wa awali Linah Jebii Kilimo na Cyrus Jirongo, Karen Nyamu miongoni mwa wengine.

Hizi hapa picha za hafla hiyo;