'Advices Zangu Zitafanya Ufinyweeee Bure ,'Akothee amjibu shabiki aliyetaka ushauri wake

Muhtasari
  • Akothee amjibu shabiki aliyetaka ushauri wake
  • Msanii Akothee anafahamika kwa bidii yake katika kazi yake na pia ushauri ambao amekuwa akiwapa mashabiki wake
Esther Akoth

Msanii Akothee anafahamika kwa bidii yake katika kazi yake na pia ushauri ambao amekuwa akiwapa mashabiki wake.

Lakini wakati huu alikiri kwamba hana ushauri wowote wa uhusiano wa kimapenzi, hii ni baada ya mmoja wa mashabiki wake kumuuliza ushauri kuhusu uhusiano wa kimapenzi.

Akothee alimwambia shabiki huyo kwamba anapaswa kuwauliza wanawake ambao wako katika ndoa.

Kulingana na Akothee yeye ni mpotezaji mkubwa katika uhusiano, lakini angempa ushauri kuhusu jinsi ya kuepuka umaskini.

"Hallo Akothee, jina langu ni Caroline nina mawazo, nataka ushauri wa uhusiano kutoka kwako, naweza pata nafasi ya kuzungumza nawe, nitashukuru sana," Shabiki huyo alimwambia Akothee.

Msanii huyo naye alimjibu haya;

"Uuuuwiiiio caro ,haki sina any , hapo kwa rushauri wa uhusiano ,tafadhali waulize wanawake ambao ndoa za ni thabiti,kutoka kwa moyo wangu kitu ambacho nitakushauri,inaweza tumiwa dhidi yanguπŸ™πŸ» , kuadhibiwa na sheria πŸ™πŸ»

Sasa Mimi na ma baby daddy watatu πŸ€” unaona couple goals kweli caro ? hii relationship boat haina nahodha , , Caro chunga nyumba yako ,mabaharia ni wengi ,wasikuibie mashua πŸ’ƒπŸ’ƒkusema ukweli maoni yangu mimi ni mpotezaji mkubwa katika uhusiano labda uniulize jinsi ya kukimbia umaskini πŸ’ƒπŸ’ƒπŸ€ΈπŸ€ΈAdvices Zangu Zitafanya Ufinyweeee Bure Karo πŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒ," Alisema Akothee.