Niko na madeni ya milioni 320 ila sijafilisika- Jamal Marlow Rohosafi

Amira alikuwa amedai kuwa bwanake ni mwenye vurugu na sio tajiri kama anavyojigamba mitandaoni

Muhtasari

•Wake wa Jimal wawili, Amira Marlow na mwanasoshalaiti Amber Ray wamekuwa wamekutumbuiza wakenya kwa vita ya maneno kufikia hatua ya Amber Ray kuhama kutoka Syokimau kuenda Milimani ili wasionane na mke mwenzake.

•Kwenye mahojiano na The Star, Jimal alisema kuwa alikuwa kondakta na hakuna aliyemshika mkono kufika mahali alipo.

Image: INSTAGRAM

Mwanabiashara amekuwa kivutio cha wanamitandao wengi kutokana na vita ambayo imekuwemo mitandaoni kati ya mabibi wake wawili.

Wake wa Jimal wawili, Amira Marlow na mwanasoshalaiti Amber Ray wamekuwa wamekutumbuiza wakenya kwa vita ya maneno kufikia hatua ya Amber Ray kuhama kutoka Syokimau kuenda Milimani ili wasionane na mke mwenzake.

Mapema wiki hii jumbe za kibinafsi zamke wa kwanza Amira zilifichuliwa na mwanablogu Edgar Obare.

Amira alikuwa amedai kuwa bwanake ni mwenye vurugu na sio tajiri kama anavyojigamba mitandaoni. Amira alisema kuwa Jimal ana madeni mengi kwenye mabenki.

Jimal alijitetea kutokana na madai hayo na kusema kuwa mikopo anayochokua huwa ya kusaidia biashara zake.

Kwenye mahojiano na The Star, Jimal alisema kuwa alikuwa kondakta na hakuna aliyemshika mkono kufika mahali alipo.

"Sitadanganya, huwa nachukua mikopo ili kugharamia biashara zangu. Kila mwanabiashara nchini ametoka mahali chini, lazima uchukue mikopo ili kujiinua zaidi" Jimal alisema.

Alisema kuwa ako na madeni ya shilingi milioni 320 katika mabenki matatu ila ana uhakika kwa anaweza kuyamudu.

"Niko na deni la Sh150M katika benki moja, kwingine milioni 80 na benki nyingine milioni 90. Kama una madeni ya kiwango hicho katika mabenki matatu basi lazima una mapato mazuri ya kumudu madeni hayo" Jimal alieleza.

Aliwakashifu wanaomsema kwa kuwa na madeni na kuwashauri kama wanahitaji mikopo wafike kwenye benki pia.

"Watu wanasema niko na madeni. Kweli, niko nayo na ikiwa wataka mkopo pia nenda kwenye benki. Huwa nawalipa vizuri." Alisema.

(Utafsiri; Samuel Maina)