(+Video) "Utakuwa wimbo wangu wa harusi" Akothee amwagia sifa wimbo mpya wa Bahati

Akothee pia amearifu mashabiki wake kuwa atachukua likizo ya muda mitandaoni ili kumakinika na familia

Muhtasari

•Wimbo wa kimapenzi ambao Bahati alitoa siku ya Jumatano umesisimua Madam Boss huku akiapa kuwa utakuwa wimbo wake wa harusi.

•Kwenye wimbo 'SWEET DARLING', Bahati alimshirikisha mpenzi wake Diana Marua kwenye video iliyosheheniwa na mahaba tele.

Akothee na Nelly Oaks
Akothee na Nelly Oaks
Image: INSTAGRAM

Msanii na mwanabiashara mashuhuri nchini Esther Akoth almaarufu kama Akothee ameonekana kupendezwa na wimbo wa hivi karibuni wa Bahati.

Wimbo wa kimapenzi ambao Bahati alitoa siku ya Jumatano umesisimua Madam Boss huku akiapa kuwa utakuwa wimbo wake wa harusi.

"Mapenzi ni kitu nzuri sana. Kila mwanamke anafaa kuwa na mwanaune anayemfanya kujihisi bora na si ambaye anamsababishia msongo wa mawazo. Huu utakuwa wimbo wangu wa harusi" Akothee alisema.

Kwenye wimbo 'SWEET DARLING', Bahati alimshirikisha mpenzi wake Diana Marua kwenye video iliyosheheniwa na mahaba tele.

BAHATI LOVE LIKE THIS ALBUM NOW AVAILABLE ON ALL STREAMING PLATFORMS! BOOMPLAY MUSIC LINK CLICK http://Boom.lnk.to/BahatiLoveLikeThis... BAHATI & SAT - B SONG : SWEET DARLING AUDIO: MESESI & TEDDY B VIDEO DIRECTOR: NEZZOH MONTANA SHOT IN KENYA & BURUNDI LABEL : EMB ENTERTAINMENT #Bahati #SweetDarling #LoveLikeThisAlbum

Kupitia ujumbe mwingine, Akothee amearifu mashabiki wake kuwa atachukua likizo ya muda  mitandaoni.

Msanii huyo alitangaza kuwa alikuwa ametimiza yote ambayo alikuwa ameombea na atachukua muda kupumzika kutoka kwa mazoezi yake ya kawaida na mitandao na kwa sasa anataka kumakinika na familia yake.

Siku za hivi Karibuni mama huyo wa watoto watano amekuwa akipakia picha akiwa pamoja na aliyekuwa meneja wake, Nelly Oaks na kuziambatanisha na jumbe za kimapenzi.

Kwenye ujumbe mmoja, Akothee alimbwagia sifa Oaks huku akijigamba vile huwa anatunzwa kama msichana mdogo naye.

"Mwanaume ambaye peke huwa hajalishwi Akothee ni nani. Mimi ni msichana maalum machoni mwake. Anaweza niambia chochote kwa wakati wowote. Umaarufu pelekea mashabiki, mwenzngu Nelly Oaks" Akothee aliandika.