Size 8 asema haya baada ya kibao chake kuchezwa katika mashindano ya olimpiki ya Tokyo

Muhtasari
  • Size 8 avunja kimya baada ya kibao chake kuchezwa Japan Tokyo
  • Safari ya usanii ya msanii huyo inafahamika sana na wanamitandao
  • Licha ya changamoto ambazo wasanii wa kike hupitia kwenye tasnia ya burudani, msanii huyo ameonekana mara kwa mara akitia bidii katika kazi yake
Size 8
Image: maktaba

Msanii mashuhuri na mshindi wa tuzo tofauti msanii wa Injili Linet Munyali anayefahamika zaidi kwa jina la Size 8 yuko na furaha baada ya kibao chake kinachofahamika kama 'Mateke' kuchezwa Japan wakati wa olimpiki Tokyo 2020.

Mama huyo wa watoto wawili aliyejawa na furaha hakuweza kuficha furaha yake baada ya Wakenya kuchukua kwenye kurasa tofauti za mitandao ya kijamii wakimkubali 'DJ wa Tokyo' kwa kumtambua Size 8.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Size 8 alisema kuwa ni kazi ya Mungu kwamba alikuwa ameenda kimataifa, na kutambulika wakati wa olimpiki.

Safari ya usanii ya msanii huyo inafahamika sana na wanamitandao.

Licha ya changamoto ambazo wasanii wa kike hupitia kwenye tasnia ya burudani, msanii huyo ameonekana mara kwa mara akitia bidii katika kazi yake.

"Uuuuwwwiiii, kibao changu cha 'Mateke' kimechezwa Japan wakati wa olimpiki za tokyo2020, ni Mungu anafanya kazi

Injili ya Yesu iko hai," Aliandika Size 8.

Aliendelea kumpongeza Mkenya Faith Kipyegon kwa kutetea taji lake la Olimpiki katika mbio za mita 1,500 za Wanawake, na kushika medali ya pili ya dhahabu kwa Kenya.

"Hingera kwa Faith Kipyegon, kwa kushinda katika mbio za mita 1,500, Mungu ni mkuu Elohim ni mkuu asifiwe Mungu aliye hai."

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

djmokenya: God is good , am so proud of you 🙌

vane_camentoh: Jesus the power that doesn't know language whenever it is mentioned must be heard❤️❤️❤️❤️🙌

anko_samie: Hii nayo I was just shocked ...size 8 ako kwa kiwanja😂

dianamoraa288: Uuuuuwi Mungu ainuliwe🙌🙌🙌

brighterca6: God can elevate you to another level