Kuna saratani-Diamond awaambia vijana baada ya kununua mkufu wa dhahabu

Muhtasari
  • Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz bila shaka ni mmoja wa watu mashuhuri zaidi ambao haogopi kutumia mamilioni ya vitu vya bei ghali na ameifanya tena
  • Kwenye ukurasa wake wa instgram aliwatangazia mashabiki kuwa amenunua mkufu mpya wa dhahabu na jina lake "Simba" limechorwa kwenye mkufu huo
Screenshot-from-2020-06-02-03_06_13
Screenshot-from-2020-06-02-03_06_13

Msanii wa Tanzania Diamond Platnumz bila shaka ni mmoja wa watu mashuhuri zaidi ambao haogopi kutumia mamilioni ya vitu vya bei ghali na ameifanya tena.

Kwenye ukurasa wake wa instgram aliwatangazia mashabiki kuwa amenunua mkufu mpya wa dhahabu na jina lake "Simba" limechorwa kwenye mkufu huo.

Kwa  miaka mingi msanii huyo amekuwa akiia bidii kattika kazi yake na katika lebo yake ambayo ni moja wapo ya lebo bora Afrika Mashariki.

Haya yanajiri karibu mwezi mmoja baada ya kununua Rolls Royce Cullinan 2021 mpya kabisa ambayo ilikadiriwa kugharimu karibu Sh30 milioni hadi Sh90 milioni, kulingana na ubadilishaji alioufanya kwenye gari.

Pia msanii huyo alifichua kuwa mkufu huo ulimgharimu USD 48,000, huku ikilinganishwa na pesa taslimu za kenya ikiwa ni milioni 5,238,595.20.

Aliwashauri vijana waache kuvalia mikufu bandia kwani kuna saratani.

" Dhahabu na AlmasiπŸ’Ž #HalfManHalfLion  acheni kuvaa mkufu bandia wavulana wadogo ... kuna saratani ✌🏼....USD 48,000…Tsh! 111,360,000 Aye ye ye! Naondokaje sasa???kwanza nawahi nini wakati nimeachwa????" Aliandika Diamond.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki;

romyjons: HALAFU KANSA YA SHINGO MBAYA SANA UNAKATWA KICHWA 😒😒😒😒😒

zikymtanah: Watu wanavaaa mbwakin sana kitaaniπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ 🦁🦁🦁

bigpapa_m10: Utaziwkwa nao hio chain? Muogope mungu

queen_msukuma: Million 40 ya original kitu kidogo nanunua kiwanja najenga naweka wapangaj maisha yanaenda huku nanunua feki ikipauka natupa πŸ˜‚

djnina___: Kwahiyo ni tutapata cancerπŸ€”

ankoo_zumo_: SIMBAA KAKA UTAUA πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ™ŒπŸ™Œ