Mama yangu ameuwa akinishauri nitoke kwa ndoa yangu niende kwa mwanamume mwingine-Mwanamke asema

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia jinsi mama yake anataka atoke kwenye ndoa yake
sad woman
sad woman

Kabla sijaandika mengi wala kusema mengi, baadhi ya wazazi wetu wanapaswa kuacha wanawe waish kwenye ndoa zao kwa amani.

Ndio ni furaha ya kila mzazi kuona mwanawe anaendelea vyema katika ndoa yake na wala hamana vurugu yoyote.

Lakini kuna wale wanapenda kuingilia ndoa za watoto wao, na kuvunja ndoa hizo mwishowe kuwaacha wateseke.

Mwanamke mmoja aliwaacha mashabiki wa radiojambo, na msahangao baada ya kifichua jinsi mama yake amekuwa akimshauri atoke kwenye ndoa yake.

Sababu kuu ya kumwambia ni nini, kulingana na mwanamke huyo, mama yake anamshauri hayo kwani hana mtoto na mumewe ilhali anahitaji mjukuu.

"Mama yangu amekuwa akinishauri nitoke kwenye ndoa yangu au niachanae na mume wangu, ili niende kwa mwanamume mwingine 

Sababu yake ni kuwa sina mtoto na mume wangu, mume wangu alinioa nikiwa na mtoto mmoja

Ameshinda kunishnikiza kuwwa anataka mjukuu mwingine, niache kuringa na mtoto mmoja anaweza kuaga dunia," Alisimulia.