"Pewa mimba yako uachane na za wengine" Guardian Angel aghadhabishwa na shabiki aliyekejeli kipenzi chake

Muhtasari

• Mwanamuziki huyo ambaye ana umri 30 amekuwa akikosolewa sana mitandaoni tangu atangaze uhusiano wake na  Bi Esther Musila mwenye umri wa miaka 51.

•Shabiki mmoja haswa ambaye ujumbe wake haukufurahisha wanamitandao wengi ikiwemo Guardian Angel mwenyewe alitilia shaka uwezo wa Bi Musila wa kubeba ujauzito.

Image: INSTAGRAM// GUARDIAN ANGEL

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Peter Omwaka maarufu kama Guardian Angel ameendelea kutetea uhusiano wake na mkewe Esther Musila.

 Mwanamuziki huyo ambaye ana umri 30 amekuwa akikosolewa sana mitandaoni tangu atangaze uhusiano wake na  Bi Esther Musila mwenye umri wa miaka 51.

Baadhi ya wanamitandao walidai kwamba Guardian Angel alijitosa kwenye uhusiano huo kwa minajili ya pesa, madai ambayo amepuuzilia mbali na kuendelea kusisitiza kwamba uhusiano kati yake na Musila umejengwa kwa msingi wa mapenzi.

Takriban wiki moja iliyopita msanii huyo alidai kwamba alitia maskio yake pamba wakati watu walikuwa wanakosoa uamuzi wake wa kuchumbia Bi Musila huku akisema kwamba iwapo angewaskiza watu angepoteza zawadi maalum.

"Kama ningeskiza kelele za watu ningepoteza zawadi maalum. Najivunia"  Guardian Angel aliandika chini ya picha ambayo alikuwa amepigwa pamoja na mkewe.

Siku ya Jumatatu Guardian Angel alipakia video ya mpenzi wake kwenye ukurasa wake wa Instagram na kama  kawaida hapakukosa baadhi ya mashabiki wa kumkosoa kutokana na uamuzi ambao alifanya mwaka uliopita.

Shabiki mmoja haswa ambaye ujumbe wake haukufurahisha wanamitandao wengi ikiwemo Guardian Angel mwenyewe alitilia shaka uwezo wa Bi Musila wa kubeba ujauzito.

"Huyu mama ukimpea mimba anaweza shika kweli? Nauliza kwa niaba ya Wakenya wenzangu" Mtumizi wa Instagram kwa jina @officialkuju alimuuliza Guardian Angel.

Mwanamuziki huyo hakusita kumjibu shabiki yule wa kike huku akimshauri awache kuwashwa na pilipili ambayo hali.

"Pewa mimba yako uachane na za wengine" Guardian Angel alimjibu shabiki huyo.

Mashabiki wengi ambao walighadhabishwa na ujumbe wa mwanadada huyo walijumuika kumkosoa na kulaani kitendo chake.

@wahukagwi Nasikitika nikiona wanawake wakijaribu kuangusha wanawake wengine.. Maumivu ambayo unashuhudia usiyasambaze kwa wengine

@mainakageni @guardianangelglobal hakuna haja ya kujibu.. uko na furaha , yeye hana.. bado unashinda!!

@marymaricengari ni jambo la aibu mwanamke kuuliza mwanamke mwingine swali kama hilo

@askari_msafi sema unauliza kwa niaba yako na wajinga wenzako kumbaf kabisa