Mungu amekuwa mwaminifu kwangu,' Daddy Owen kuzindua albamu yake ya 6 Oktoba

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili Daddy Owen ametangaza uwa atazindua albamu yake ya 6 Oktoba 16 2021
daddy owen
daddy owen

Msanii wa nyimbo za injili Daddy Owen ametangaza uwa atazindua albamu yake ya 6 Oktoba 16 2021.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo amesema kwamba licha ya magumu aliyoyapitia Mungu amekuwa mwaminifu kwake.

"OKTOBA 16? kila mtu amekuwa akiuliza .. jibu hapa! Tangu mwaka jana wakati nilikuwa nikipitia maswala ya kibinafsi niliamua kuanza safari katika studio kuandika na kurekodi Albamu yangu ya 6, imekuwa safari .. kihemko, Kiroho na Kimwili.

MUNGU amekuwa mwaminifu kwangu kwamba sasa ninawasilisha kwako albamu mpya SURA YA 4 ambayo inaweza kuzinduliwa tarehe 16 Oktoba !!

Ninaandika machozi haya ya kusawazisha kwa sababu najua jinsi safari imekuwa ngumu .. ninachoweza kusema ni kwamba YESU NI MJASIRIAMALI πŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ," Aliandika Owen.

Mapema mwaka huu Owen akiwa kwenye mahojiano alifichua kwamba amekuwa akipambana na msongo wa mawazo, ila aliogopa kusema kwani aliona ata atakejeliwa na wanamitandao.