'Mke wangu ndiye Mali ya bei ghali zaidi ninayomiliki hivi sasa,'Jimal Roho Safi afichua

Muhtasari
  • Mfanyibiashara Jimal Roho Safi alifahamika sana baada a kumuoa mwanasosholaiti Amber Ray mapema mwaka huu

Mfanyibiashara Jimal Roho Safi alifahamika sana baada a kumuoa mwanasosholaiti Amber Ray mapema mwaka huu.

Uhusiano wao ulikuwa na vizuizi vingi kwani alikuwa na mke wa kwanza,ambaye wamebarikiwa naye watoto wawili.

Akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo Amira alisema kwamba alifahamu uhusiano wa mumewe na Amber kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya uhusiano wake na Amber Ray kuisha, Jimal alimrudia mke wake wa kwanza na ambaye amekuwa akimridhisha kwa kila jambo ili kumuomba msamaha kwa yale yalitokea.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram , Jimal alijibu swali ambalo aliulizwa nini haswa kitu cha bei ghali anachomiliki kwa sasa.

Kulingana na Jimal Mali ya bei ghali zaidi ninayomiliki hivi sasa ni mke wake;

"Ni mali ipi ghali zaidi unayomiliki sasa?"

Mimi Mke wangu,"Jimal alijibu.

Tunatumai ndoa yake Jimal na mkewe itaendelea, na mapenzi yao yataendelea kunoga kila kuchao.