"Hali hii inatisha!" Akothee azungumza kuhusu ugonjwa unaomwathiri ambao umefanya avimbe na kuonekana mnene zaidi

Muhtasari

•Akothee amesema maumivu ambayo amekuwa akipata mwilini yamemfanya kukosa usingizi kiasi cha kwamba amekuwa akihofia kuingia kitandani.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mfanyibiashara mashuhuri Esther Akoth almaarufu kama Akothee amewasuta wanaokosoa mabadiliko ambayo yamejitokeza mwilini wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mama huyo wa watoto watano amesema anaonekana mnene kutokana na uvimbe uliosababishwa na hali ya afya ambayo imemwathiri kwa muda sasa.

Akothee amesema maumivu ambayo amekuwa akipata mwilini yamemfanya kukosa usingizi kiasi cha kwamba amekuwa akihofia kuingia kitandani.

'Usikutane na kuanza kuniambia jinsi nilivyo mnene, nina hali ya kiafya, nimevimba kutokana na kuhangaika na maumivu ya kukosa usingizi, naogopa kwenda kulala maana ninaamka na ganzi kwenye vidole vyangu, hali hii inanitisha. Namuonea huruma jamaa yangu mmoja wa karibu aliyesema najifanya  bado sijui nimwambie nini " Akothee amesema.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 41 amewasuta vikali wanaomtakia maovu na kuongea mabaya kuhusu hali yake huku  akidai sanasana watu wenye tabia ile huwa wale wa karibu.

"Kwani niko shule ya bweni nahitaji ruhusa ya kwenda nyumbani ? ! Au hata mimi namhurumia nani? Je, mimi ni mfanyakazi, ninaweza kupata muda wa kupumzika na familia yangu na kutoenda kazini  Wao! kama kuna yeyote anayekutakia mabaya ni watu unaowaweka karibu na moyo wako, waombee hata hivyo" Amesema Akothee.

Wiki mbili zilizopita Akothee alipatiwa ruhusa kutoka hospitalini ambako alikuwa amelazwa kwa siku kadhaa baada ya kulalamika kuhusu maumivu mwilini.

Baada ya kuondoka hospitali mwanamuziki huyo alimlimbikizia sifa kochokocho mpenzi wake Nelly Oaks kwa kusimama naye wakati wa maumivu yake.