Ujumbe wa Lilian Ng'ang'a kwa Diana Marua baada ya kijitosa kwenye tasnia ya muziki

Muhtasari
  • Ujumbe wa Lilian Ng'ang'a kwa Diana Marua baada ya kijitosa kwenye tasnia ya muziki
Image: INSTAGRAM// LILIAN NGANGA

 Lillian Nganga amejitokeza kumuunga mkono Diana Marua baada ya kuanza rasmi safari yake ya muziki.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Lillian aliwakumbusha mashabiki wake kwamba mtu yeyote anaweza kuwa chochote anachotaka kuwa ikiwa kuna nia na dhamira.

Akimtakia Diana Marua mafanikio katika safari yake mpya, Lillian alimwomba ajitoe bora zaidi na kuhakikisha anakuwa toleo bora kwake.

Kauli yake inajiri muda mfupi baada ya mwimbaji mwenye utata Esther Akoth almaarufu Akothee pia kutoa msaada wake kwa Diana.

"KIla mmoja wetu anaweza kuwa kile anataka kuwa, Diana Marua, kuwa kile chote unataka kuwa chote," Aliandika Lilian.

Akichagua vazi la Diana ambalo limekuwa gumzo, Akothee alisema kuwa hakuna ubaya nalo, na kama angekuwa yeye, angechagua vazi fupi zaidi.

Pia alimwomba Diana asizingatie mambo hasi yanayotokana na wenye chuki.

Yote Haya yanajiri baada ya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kumkashifu Diana, wakipuuza uamuzi wake wa kujitosa kwenye muziki.

Je kibao chake Diana kimeweza au hakijaweza?