Baadhi ya watu mashuhuri ambao wamepambana na hali ngumu mwaka wa 2021

Muhtasari

•Katika makala haya tutaangazia baadhi ya watu mashuhuri nchini ambao wamepambana na maradhi mabaya mwaka huu.

Moses Kuria, King Kaka, Akothee
Moses Kuria, King Kaka, Akothee
Image: HISANI

Hatimaye mwaka wa 2021 unakaribia kufika kikomo na hivi karibuni tutakuwa tunafungua kalenda mpya.

Mengi yametendeka tangu mwaka huu ulipoanza, mengine ya kusherehekea na mengine ya kusikitisha.

Baadhi ya watu mashuhuri wa  hapa nchini wamekuwa na mambo ya kujivunia huku wengine wakipitia mambo magumu ambayo wangetamani kuyasahau.

Katika makala haya tutaangazia baadhi ya watu mashuhuri nchini ambao wamepambana na maradhi mabaya mwaka huu.

1. King Kaka

Mwanamuziki wa nyimbo za kufoka Kennedy Ombima almaarufu kama King Kaka alikuwa anaugua kwa kipindi kirefu mapema mwaka huu.

Mnamo mwezi Septemba King Kaka alifunguka kuhusu ugonjwa wa kustaajabisha ambao ulikuwa umemwathiri kwa kipindi cha miezi mitatu.

King Kaka alisema alianza kuugua baada ya kupimwa vibaya alipoenda kupokea matibabu hospitalini baada ya kuugua kidogo.

Rapa huyo alifichua kwamba ugonjwa uliomshambulia ulimfanya apoteze zaidi ya kilo 33, kiuno chake kupungua, midomo yake kuwa nyekundu, kupoteza hisia ya ladha tutapika damu, kuendesha kati ya dalili zingine za kuogofya.

Hata hivyo, Kwa sasa baba huyo wa watoto watatu amefanikiwa kupata afueni kwa neema zake Mola na ameweza kurejelea kazi yake ya usanii.

2. Akothee

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu kama Akothee alifichua habari kuhusu kuugua kwake takriban miezi miwili iliyopita.

Katikati ya mwezi Novemba mama huyo wa watoto watano alilazwa hospitalini  baada ya maumivu kumzidia.

Akothee aliporuhusiwa kuenda nyumbani mabadiliko kadhaa yangeonekana mwilini wake. Alionekana mnene zaidi, hali ambayo alisema ilitokana na uvimbe uliosababishwa na ugonjwa ambao ulimwathiri kwa muda sasa.

Wiki chache zilizopita Akothee alifichua kwamba maradhi yaliyomshambulia yalikuwa yamefanya alazwe hospitalini mara tano.

Ingawa mwanamuziki huyo bado hajapata afueni kikamilifu, afya yake imeonekana kuwa imara zaidi kuliko ilivyokuwa takriban miezi miwili iliyopita.

Moses Kuria

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria anaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja kubwa Dubai.

Hii ni baada ya mwandani huyo wa naibu rais William Ruto kushambuliwa na ugonjwa wa kustaajabisha mnamo mwezi Septemba.

Blanketi lake la umeme ambalo lilimuacha na majeraha mabaya ya moto yaliyohitaji kulazwa hospitalini kwa muda murefu.

Kuria amefanyiwa upasuaji hapa nchini na ughaibuni mara kadhaa kufikia sasa katika juhudi za kurejesha afya yake.

Akuku Danger

Image: HISANI

 

Mchekeshaji mashuhuri Akuku Danger anaugua vibaya na kwa sasa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Inaripotiwa mchekeshaji huyo wa Churchill amekabiliwa na matatizo ya mapafu na kwa sasa pafu lake moja limeathirika vibaya.

Familia yake imeomba msaada wa fedha kutoka kwa Wakenya ili kugharamia matibabu ya msanii huyo.