'Wanawake watakutilia Sumu,'Akothee amshauri mwanawe Rue Baby jinsi ya kuishi na wanawake

Muhtasari
  • Akothee amshauri mwanawe Rue Baby jinsi ya kuishi na wanawake

Mama wa watoto 5 na mwimbaji Akothee anayejulikana kwa machapisho yake ya kutatanisha kwenye Instagram ameandika ujumbe kwa bintiye mdogo Rue Baby kuhusu jinsi ya kuishi na wanawake wanaomzunguka maishani mwake.

Mwimbaji huyo ambaye kwa sasa anatumia muda mzuri na binti yake aneo la  pwani alimwambia bintiye kwamba mwanamke anaweza fanya chochote ili kukushusha chini.

Pia alimshauri kwamba anapaswa kuwaambia hadithi tofauti, ili wabishane wao wenyewe kwa wenyewe.

"Mama ndiye mwanamke pekee rafiki ambaye anataka kukuona ukifanya vizuri zaidi yake. @rue.mtoto Wanawake wengine walio karibu nawe watakutilia sumu kwa kufikiwa na mwanaume ambaye huwapuuza! 👉Wanawake wanaweza kukutia sumu kwa kupandishwa cheo kazini kwako 👉Siku zote wasimulie hadithi mbalimbali kuhusu wewe ili wawe wanagombana na kupigana wenyewe Inaitwa MAISHA 💪ISHI ,💪," Akothee Alisema.

Akothee amekuwa akiwapa wanawe ushauri tofauti, kupitia kwenye mitandao ya kijamii, na jinsi ya kupuuza wakosaji wao mitandaoni.