'Heshimu mumeo,'Otile Brown amwambia Vera Sidika

Muhtasari
  • Vera pia alisema kwamba ataunga mkono collabo kati ya mppenzi wake Brown Mauzo na Otile iwapo wawili hao wataamua kufanya kazi pamoja

Msanii maarufu Otile Brown kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemkemea na kumwambia aliyekuwa mpenzi wake Vera Sidika ajaribu kumheshimu mumeo.

Katika ujumbe wake hakumtaja mtu ila kulingana na wanamitandao ujumbe huo ulikuwa unamwendea Vera ambaye hivi majuzi amekuwa akimtaja Otile na kusema kwamba hamna damu mbaya kati yao.

Vera pia alisema kwamba ataunga mkono collabo kati ya mppenzi wake Brown Mauzo na Otile iwapo wawili hao wataamua kufanya kazi pamoja.

"Jaribu kumheshimu mumeo na kulinda ndoa yako, kama ninavyojaribu kila unapotaja jina langu. Don’t get comfortable.”

Hii ni baada ya mmoja wa mashabiki wake kupitia kwenye insta stories kumuuliza iwapo ataunga mkono collabo kati ya Otile na mumewe Mauzo.

"Kama Otile Brown atataka kufanya collabo na mpenzi wako Brown Mauzo utaunga mkono collabo hiyo au la," Shabiki Aliuliza.

"Nitaunga mkono kwa asilimia 100, hamna kitu mbaya na hilo," Vera Alijibu.