Siwezi amini mtu na mtoto wangu-Huddah Monroe

Muhtasari
  • Visa vya vijakazi kuwatesa na kuwadhulumu watoto wa waajiri wao vimekuwa vikiripotiwa kwa muda nchini
Huddah Monroe
Image: Facebook

Je unapaswa kuzingatia nini endapo unataka kuandika kijakazi ili akulindie watoto wako wakati uko kazini?

Visa vya vijakazi kuwatesa na kuwadhulumu watoto wa waajiri wao vimekuwa vikiripotiwa kwa muda nchini.

Mwanasosholaiti maarufu nchini Huddah Mnroe kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amekiri kwamba hawezi amini mtu yeyote na mtoto wake.

Hata hivyo Huddah ameisisitiza kwamba hawezi amini hata familia yake na mwanawe.

Hivi majuzi HUddah amekuwa akiwashauri mashabiki wake hasa wa kike jinsi ya kuishi maisha yenye furaha.

Huddah alisema haya baada ya kijakazi, kufungwa kwa miaka 15 kwa kunyanyasa binti ya mwajiri wake.

"Sidhani kama naweza amini mtu na mtoto wangu hata familia labda mama yangu,ninalinda sana, ulimwengu huu ni mbaya sana, watoto hawawezi kujichunga," Huddah Aliandika.

Huku watoto wakiwa kwenye likizo, wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wao, na kufanya uchunguzi zaidi kabla ya kumwajiri kijakazi yeyote.