Bahati na Diana Marua wahamia kwenye jumba lao jipya la kifahari

Muhtasari

•Bahati alipakia video kadhaa  zilizoonyesha wahamishaji wakisaidia kuhamisha na kupanga baadhi ya vitu vyao vya nyumba.

Image: INSTAGRAM// BAHATI

Siku ya Jumatatu wanandoa mashuhuri Bahati na Diana Marua walianza hatua ya kuhamia kwenye jumba lao mpya.

Diana Marua ambaye miezi kadhaa iliyopita alizindua taaluma yake ya muziki akijitambulisha kama rapa Diana B alitangaza habari za kuhama kwao kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mama huyo wa watoto wawili alipakia video kadhaa  zilizoonyesha wahamishaji wakisaidia kuhamisha na kupanga baadhi ya vitu vyao vya nyumba.

"Kazi inaendelea.... redio imewekwa.. wanaweka redio na playstation kwenye chumba cha watoto," Diana aliandika chini ya baadhi ya video hizo.

Mwezi uliopita Bahati alimkabidhi mkewe nyumba hiyo kama zawadi ya Valentines. Kando na nyumba, mwanamuziki huyo pia alimpatia mkewe gari na shamba kusherehekea mapenzi yao.

Diana alimshukuru sana mumewe kwa zawadi ya nyumba hiyo huku akisema kuwa ndiyo zawadi bora zaidi ya Valentines ambayo amewahi kupokea.

Wawili hao wanajulikana kununuliana zawadi za dhamani katika siku maalum kama maadhimisho ya siku ya kuzaliwa, maadhimisho ya ndoa, Valentines n.k.