Ringtone adai alimpeleka DJ MO Amerika kwa mara ya kwanza

Muhtasari

• Ringtone anasema kwamba safari ya kwanza kwa DJ Mo kuelekea na kutia guu lake katika udongo wa Marekani ilifadhiliwa na yeye.

Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

Mwenyekiti wa muziki wa injili nchini Kenya kama anavyojiita mwenyewe RAington anasemac kwamba yeye ndiye aliyempeleka mcheza santuri wa injili DJ Mo Marekani kwa mara ya kwanza kabla hata watu wamjue.

Rington anasema kwamba safari ya kwanza kwa DJ Mo kuelekea na kutia guu lake katika udongo wa Marekani ilifadhiliwa na yeye.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na mchekeshaji na mkuza maudhui wa mtandao wa YouTube, Dr. Ofweneke, Rington alisema kwamba yeye ni tajiri kumliko DJ Mo na familia yake kwa ujumla na kusema kwamba hata kama juzi alionekana akimfukuza kutoka kwa hafla ya uzinduzi wa albamu ya mkewe Size 8, lakini itabakia kuwa ukweli kwamba bila yeye pengine DJ Mo hangewahi fika Marekani.

“Mimi ndio nilipeleka DJ Mo Amerika the first time. DJ Mo hangewahi fika Amerika kama si mimi. Nilikuwa nimepewa invitation kwa event na Wakenya kule Amerika. Mimi nili offer na kuwa-beg hao Wakenya waliokuwa wameniita kwa event iliyokuwa inaitwa Talanta Awards, niliwaomba tafadhali acha Alemba na Mo waniwakilishe kwa sababu nilikuwa nasimama kiti cha siasa pale Kisii. Na mimi ndio niliwapeleka hata nika-organise documents walikuwa wanatakiwa kuwa nazo within a week. Wakaenda, na sijawahi sikia wamepost mahali popote wakisema Ringtone thanks ulitufikisha Amerika,” alisema Ringtone.

Msanii huyo alisema kwa sababu Mo hakuwahi mpa shukrani ndio maana aliimba collabo na msanii mkubwa wa injili kutoka Tanazania, Christine Shusho, kwa jina Tenda Wema Nenda Zako.