Kuamini mtu hakuna thamani-Amber Ray asema

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti huyo alivuma sana baada ya kuolewa na mfanyibiashara Jimal Roho Safi huku wakiachana baada ya muda mfupi
Amber Ray
Image: Hisani

Amber Ray amekuwa mmoja wa mastaa wa kike wenye ushawishi mkubwa nchini.

Hata hivyo, yeye pia ni mmoja wa wanasosholaiti wengi ambao kila mara hujihusisha na mabishano ambayo wakati mwingine husababisha migogoro ya mitandaoni na baadhi ya wafuasi wake mitandaoni.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Amber amekuwa akiwashauri mashabiki wake,huku siku ya Ijumaa akisema kwamba kumuamini mtu hakuna thamani yeyote.

Mwanasosholaiti huyo alivuma sana baada ya kuolewa na mfanyibiashara Jimal Roho Safi huku wakiachana baada ya muda mfupi.

"Si msaada wote unahusisha pesa, kuamini mtu hakuna thamani. Okoth asante kwa kuamini chapa yangu," Amber Aliandika.

Ujumbe wake ulivutia wengi wa mashabiki wake huku wakitoa hisia zifuatazo;

rosebellaharry: Wale wakusema ni uchawi kwa inbox wataambia watu nini😮😮😮

okoth.poetica: You're most welcome Amber. The wise call it Social Capital. With thanks 😊🙏🏿

oluochdaisy: Keep going sweety 😍