Lala salama!Msanii Joyce Omondi ampoteza dada yake

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili na mtangazaji Joyce Omondi anaomboleza kufuatia kifo cha dada yake mdogo
Joyce Omondi
Image: Facebook

Msanii wa nyimbo za injili na mtangazaji Joyce Omondi anaomboleza kufuatia kifo cha dada yake mdogo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagrama msanii huyo aliandika ujumbe mrefu uliosoma;

"Nimeanza na kufuta sentensi hii ya kwanza mara nyingi zaidi kuliko ninavyoweza kuhesabu kwa sababu ninahisi kufa ganzi na kukosa la kusema.

Ni vigumu sana kujaribu kukubali kwamba dada yetu mdogo mrembo,  Gathoni, ghafla hayuko nasi tena. Hatujawahi kufikiria hasara kama hiyo ...

Ee Bwana, tunakukazia macho. Mfalme wetu mfufuka, Wewe tu, upendo wako usio na kikomo na neema ya kutosha ndio jibu la maumivu na huzuni hii."

Joyce alisema kwamba matumaini yake yako kwa Mungu hasa wakati huu wanapitia wakati mgumu.

"Katika Kristo pekee tumaini langu linapatikana Yeye ni nuru yangu, nguvu zangu, wimbo wangu Jiwe hili la msingi, ardhi hii thabiti Imara katika ukame na dhoruba kali zaidi Ni urefu gani wa upendo, ni kina gani cha amani Hofu inapotulia, mapambano yanapokoma Mfariji wangu, yote yangu katika yote Hapa katika upendo wa Kristo nasimama"