Sarah Kabu afichua ndiye aliyependekeza jina la mwanawe Diana Marua

Muhtasari
  • Afisa mkuu mtendaji wa Bonifire Adventure leo amefichulia umma kuwa yeye ndiye aliyemsaidia Diana kuchukua jina la Malaika
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mjasirimali, Sarah Kabu amefichulia umma kwamba yeye ndiye aliyemsaidia Diana marua kumpa jina mtoto wake mdogo.

Akiongea kupitia jukwaa la Instagram dakika chache baada ya Diana kupakia picha ya mtoto wake, mwanadada huyo maarufu alisema kuwa yeye ndiye aliyependekeza jina la Malaika kwa binti yao.

Wakizungumza kupitia mitandao ya kijamii, Bahati na mkewe hivi majuzi walifichua kwamba wangependa mapendekezo kadhaa kwa ajili ya jina la binti yao.

Afisa mkuu mtendaji wa Bonifire Adventure leo amefichulia umma kuwa yeye ndiye aliyemsaidia Diana kuchukua jina la Malaika.

"Congratulations @diana_marua and @bahatikenya 🎊 👏 💐 team Dee finally my name won their hearts🏆 🙌 👏 baby @malaika_bahati welcome to the world 🌎 we love u ❤️ aki am getting serious baby fever😢karibu nikuimbie karibu kenya hakuna matata😍,"Sarah Aliandika.

Baadhi ya wanamtandao walisema jinsi Sarah alivyo mbunifu kulifikiria jina hilo huku wengine wakidai kuwa hawajui kuwa watu hao mashuhuri ni wa karibu kiasi hicho.