Mchumba wa Amber Ray azungumzia sababu ya kutengana naye akiwa mjamzito

Rapudo aliweka wazi kwamba ukweli utajidhihirisha hivi karibuni.

Muhtasari

•Amber Ray alithibitisha mwisho wa mahusiano yake na Rapudo ya miezi michache siku ya Jumatano asubuhi.

•Rapudo alidokeza kuwa kuna uwongo fulani ndani ya mahusiano yake  na mwanasosholaiti huyo maarufu.

Amber Ray na Kennedy Rapudo
Image: INSTAGRAM// AMBER RAY

Mfanyibiashara mashuhuri Kennedy Rapudo amesema kwamba sababu ya yeye kutengana na mwanasoshalaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray itabainika wazi katika kipindi cha chini ya miezi miwili ijayo.

Amber Ray alithibitisha mwisho wa mahusiano yao ya miezi michache siku ya Jumatano asubuhi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Katika chapisho lake, mama huyo wa mvulana mmoja alitangaza kwamba yuko single huku akibainisha kuwa amechoshwa na mapenzi.

"Ni siku mpya ya kuanza kama mama single wa watoto wawili. Nimechoka na mapenzi," Amber Ray alisema.

Aliongeza, "Ni asubuhi, giza itaingia."

Kwa upande wake, Rapudo alisema  hatafichua mengi kuhusu kile kilichotokea lakini akaweka wazi kuwa ukweli utajidhihirisha hivi karibuni.

Katika taarifa yake ya Instagram, alidokeza kuwa kuna uwongo fulani ndani ya mahusiano yake  na mwanasosholaiti huyo maarufu.

"Uongo una tofauti nyingi, ukweli hauna hata moja. Katika muda usiozidi miezi miwili, sote tutajua ukweli na sababu ya kuvunjika kwa mahusiano. Ni hayo tu kwa sasa," mfanyibiasha huyo alisema Jumatano asubuhi.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya wawili hao kuandaa karamu kubwa ya kufichua jinsia ya mtoto ambaye wanatarajia.

Hapo awali, pia walikuwa wameachana kwa muda mfupi na kuacha kufuatiliana kwenye Instagram. Rapudo wakati huo alisema walikuwa wakikabiliana na panda shuka kama mahusiano mengine yoyote.

 "Ili tu kuzungumzia wasiwasi na uvumi. Si kwamba nina deni la maelezo kwa mtu yeyote. Hapana, hatujaachana na kwa wakati huu, sidhani kama hiyo inaweza kuonekana. Ndiyo kama uhusiano mwingine wowote, sisi huwa na heka heka zetu lakini huwa tunajaribu kusuluhisha mambo yetu,” alifafanua.

Mapema mwezi huu, baba huyo wa msichana mmoja aliibua maswali mengi kuhusu hali halisi ya mahusiano yao. Hii ni baada ya kuchukua hatua ya kufuta picha zote za Amber Ray ambazo alikuwa amepakia kwenye Instagram.

Baadaye aliachia ujumbe wenye ukakasi kwenye instastory yake – kiashiria kwamba huenda mambo si mazuri katika uhusiano wao.

"Wakati mwingine kuendelea kung’ang’ania jambo kunaleta madhara makubwa kuliko kuliachia liende vile linaenda tu," Alisema.

Rapudo alimvisha mwanasoshalaiti huyo pete ya uchumba mwishoni mwa mwaka jana jijini Dubai ambako walikuwa wameenda likizo.

Wawili hao walijitosa kwenye mahusiano ya kimapenzi katikati mwa mwaka jana baada ya kuwa marafiki kwa muda.