Kula dawa ya mdomo wako,'Msanii Willy Paul amkejeli Ringtone baada ya kuchapwa

Muhtasari
  • Msanii Willy Paul amkejeli Ringtone baada ya kuchapwa
  • Msanii Willy Paul na Ringtone wamekuwa maadui kwa muda sasa, baada ya Ringtone kuchapwa na mwanablogu Alai, Willy alimkejeli na kudai kwamba amepkea dawa ya mdomo wake

Msanii Willy Paul na Ringtone wamekuwa maadui kwa muda sasa, baada ya Ringtone kuchapwa na mwanablogu Alai, Willy alimkejeli na kudai kwamba amepkea dawa ya mdomo wake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Msanii huyo pia amekiri kwamba hawajakuwa kwenye uhusiano mzuri wala kupendana wakiwa na Ringtone.

"Nani amepiga Ringtone Rungu? Si poa, Ringtone unajua mimi na wewe hatuko sawa. Hatupendani, sikupendi, haunipendi. But chenye umepitia, umepachikwa rungu ya komeo. Umama, kula dawa ya mdomo wako," Willy alisma huku akicheka.

Baada ya kutibiwa Ringtone aliwashukuru mashabiki kwa maombi yao na kusema kwamba anasubiri sheria ichukue mkondo wake.

Alifichua kwamba alikuwa ametoka nje ya hospitali ya Kenyatta ambapo alitibiwa baada ya kuchukua p3.

"Nataka kuwashukuru Wakenya wote ambao waliniombea baada ya shambulio na pia nataka kuwashukuru madaktari wa hospitali ya Kenyatta ambao walinitibu Nataka tu mashabiki waendelee kuniombea, "alisema.