'Mko na upuzi!' Karen Nyamu awashambulia mashabiki waliomkejeli kwa kuimba kibao cha Samidoh

Muhtasari
  • Karen Nyamu awashambulia mashabiki waliomkejeli kwa kuimba kibao cha Samidoh

Mwanasiasa Karen Nyamu kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewakashifu na kuwashambulia wanamitandao ambao wamekuwa wakimkejeli akiimba kibao cha baba wa mtoto wake Samidoh.

Mapema mwaka huu wawili hao waligonga vichwa vya habari baada ya kuthibitisha kwamba wana mtoto pamoja.

Wanamitandao ya kijamii walimlaumu yeye na Samidoh kwa kumuumiza mke wa kwanza wa Samidoh.

''Mko na upuzi. So, you people can sing to Samidoh's songs the way you want, but when I sing, it becomes violence?. [nyinyi mnaeza imba wimbo wa baba Sam vile mnataka , mimi nikiimba ni vayolence.] You are all mad. Yes you. Or you think he is a deadbeat, he disowned his son like most of your baby daddy?. I am not laughing at you but your brains are empty.'' Aliandika NYamu.

Ingawa mwimbaji huyo aliomba msamaha kwa mkewe wa kwanza, Karen ameshtumiwa kwa sababu ya kukataa kutoka kwake.

Wana mtoto pamoja na haijulikanikama wanasaidiana kumlea mtoto wao au la.