Vera Sidika aapa kupatia bintiye malezi bora, amnunulia kitanda cha 300,000 na kufanya 'baby shower' ya 800,000

Muhtasari

•Mama huyo mtarajiwa amedai kuwa sherehe ambayo alifanya ndiyo bora zaidi ashawahi kuhudhuria na kueleza kuwa ilimgharimu zaidi ya shilingi laki nane.

•Mpenzi huyo wa Mauzo ameapa kuwa ako tayari kufanya lolote kupatia binti ambaye anatarajia kujifungua malezi bora zaidi.

•Mwanasoshalaiti huyo amesema kuwa bintiye atakuwa jasiri kama yeye na hataogopa kukabiliana na yeyote.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti mashuhuri nchini Vera Sidika pamoja na mpenzi wake mwanamuziki Brown Mauzo  wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja hivi karibuni.

Siku ya Jumapili mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31 alifanya sherehe kubwa ya matayarisho ya hatua ya kuitwa mama maarufu kama 'baby shower' ambayo amedai ilimgharibu pesa nyingi sana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mama huyo mtarajiwa amedai kuwa sherehe ambayo alifanya ndiyo bora zaidi ashawahi kuhudhuria na kueleza kuwa ilimgharimu zaidi ya shilingi laki nane.

Vera alifichua gharama ya sherehe hiyo alipokuwa anakosoa baadhi ya wanaitandao amba o walidai kuwa alichangisha pesa za kufanya maandalizi ya sherehe hiyo.

"Niambieni, binadamu kama mimi anawezaje tumia shilingi 113, 000 ambazo sikuomba kufanya sherehe maridadi ya baby shower ambayo ilinigharimu zaidi ya 800k kwa kuwa nyinyi wote mnasema eti watu walichanga pesa za baby shower" Vera alisema.

Mpenzi huyo wa Mauzo ameapa kuwa ako tayari kufanya lolote kupatia binti ambaye anatarajia kujifungua malezi bora zaidi.

Amefichua kuwa tayari ameagizia bintiye kitanda cha mtoto  kutoka Uingereza ambacho kimemgharimu shilingi laki tatu za Kenya.

"Nitafanya makubwa na zaidi kwa atakayekuwa binti yangu. Nilihakikisha kuwa nilimfanyia baby shower nzuri zaidi!! Haki ya Mungu!! Atatazama video hizi siku za usoni  na afurahie kuwa nilimfanyia sherehe bora

Kitanda chake pekee kilinigharimu shilingi 300,000 kutoka Uingereza." Alifichua Vera.

Mwanasoshalaiti huyo amesema kuwa bintiye atakuwa jasiri kama yeye na hataogopa kukabiliana  na yeyote.

"Binti yetu atakuwa jasiri kama mama yake. Hakuna atakayemwambia kitu!!  Atawanyoosha kweli kweli" Vera alidai.