'Wanapendeza sana,' Fayvanny azungumzia uhusiano wake na mpenzi wa sasa wa baby daddy wake Rayvanny, Paula Kajala

Muhtasari

•Fayvanny alisema kwamba kamwe hajawahi kuchochea ugomvi wowote dhidi ya mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 19 licha ya kuwa  hapo awali Paula mwenyewe ameonekana akmrushia vijembe mara kadhaa mitandaoni.

•Alikiri kwamba moyo wake ulivunjika na alilia sana wakati Rayvanny alitambulisha Paula Kajala kama mpenzi wake mpya siku ya Valentines mwaka huu  kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Image: INSTAGRAM

Aliyekuwa mpenzi wa Rayvanny na ambaye wana mtoto mmoja pamoja Fahima almaarufu kama Fayvanny amefunguka kuhusu uhusiano wake na mpenzi wa sasa wa nyota huyo wa Bongo Paula Kajala.

Alipokuwa kwenye mahojiano na Wasafi Media hivi karibuni, Fayvanny alisisitiza kwamba wametengana kabisa na staa huyo ila akaweka wazi kwamba sio binti ya mwigizaji Fridah Kajala, Paula aliyesababisha kuvunjika kwa ndoa yao.

Fayvanny alisema kwamba kamwe hajawahi kuchochea ugomvi wowote dhidi ya mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 19 licha ya kuwa  hapo awali Paula mwenyewe ameonekana akmrushia vijembe mara kadhaa mitandaoni.

"Tuliachana na Rayvanny, niko na uhakika. Paula hakufanya tuachane na Rayvanny. Mimi sijawahi kuandika chochote dhidi yake. Labda yeye anamrushia mwanaume mwingine, unajua mwanaume ni yuleyule anaweza kuwa na watu wengi" Fayvanny alieleza.

 Mfanyibiashara huyo mashuhuri Bongo alisema kwamba hakuna mawasiliano ambayo yanaendelea kati yake na Paula  kwa sasa ila akaeleza kuwa huenda shughuli zao nyingi ndizo hufanya wasiwasiliane.

Hata hivyo alifichua wamewahi kufanya biashara pamoja ila haikufanikiwa.

"Mwanzoni yeye ndiye aliyenitafuta. Alitaka bidhaa kutoka kwa duka yangu na akaniambia nimfuate. Hatukufikia kwenye hatua ya kuuziana kabisa kwa sababu kuna vitu alitaka nimletee, nikaagiza nikanunua ila mwisho wa siku akaniambia eti pesa yake haitoshi. Aliseman atachukua wakati mwingine" Fayvanny alisimulia.

Mama huyo wa mtoto mmoja alikiri kwamba moyo wake ulivunjika na alilia sana wakati Rayvanny alitambulisha Paula Kajala kama mpenzi wake mpya siku ya Valentines mwaka huu  kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

"Nilisema asante Mungu, ijapokuwa iliniuma sana lakini nikaona sina sababu ya kuumia. Nilisema asante Mungu  wewe ndio ulimleta na ukamchukua. Nililia sitakuwa muongo. Niliumia sana" Alikiri Fayvanny.

Hata hivyo amesema kwamba anawasherehekea mahusiano yao huku akidai kwamba wanapendeza sana pamoja. 

Licha ya kwamba wana mtoto wa miaka minne pamoja, Fayvanny aliwatakia Rayvanny na Paula mahusiano marefu.

"Niliyapokea  mahusiano yao vizuri , wanapendeza sana.. nawasherehekea sana na natarajia kuwaona mbali wasiishie tu  njiani"  Fahvanny alisema.

Kwa sasa Paula ako nchini Uturuki kuendeleza masomo yake.