Mwigizaji Robert Agengo afichua amepata watoto 6 na wanawake 5 tofauti, aeleza namna huwa anawamudu

Muhtasari

•Mwigizaji huyo alifichua kwamba yeye ni baba ya watoto sita ambao amepata na wanadada watano tofauti.

•Mwigizaji huyo alisema kuwa kukimu mahitaji ya watoto wake wote sio rahisi ila huwa anajaribu wajibika kadri awezavyo.

•Kulingana na Agengo, sio sharti mwanaume awe na uwezo wa kifedha ili awe na uhusiano mzuri na mtoto wake.

Image: INSTAGRAM// ROBERT AGENGO

Mwigizaji mashuhuri nchini Robert Agengo amefunguka kuhusu familia yake kubwa na kueleza jinsi huwa anawamudu.

Alipokuwa kwenye mahojiano na Buzz Central Kenya hivi karibuni, mwigizaji huyo alifichua kwamba yeye ni baba ya watoto sita ambao amepata na wanadada watano tofauti.

Agengo ambaye anafahamika zaidi kutokana na kipindi cha Zora alieleza kuwa kati ya wanadada ambao amepata watoto nao, mmoja ako na watoto wake wawili ilhali wengine wanne wako na mtoto mmoja wake kila mmoja wao.

"Niko na watoto sita. Mwanamke wa kwanza alipata watoto wangu wawili. Wengine wanne wako na mtoto mmoja kila mmoja wao" Agengo alikiri.

Agengo alisema kwamba mtoto wake wa tatu na wanne walizaliwa mwaka mmoja na wanawake wawili tofauti

Mwigizaji huyo alisema kuwa kukimu mahitaji ya watoto wake wote sio rahisi ila huwa anajaribu wajibika kadri awezavyo.

"Saa zingine tunasumbuana na baby mamas. Kama unajua maisha ya usanii ya ukweli utajua namna hali itakuwa. Tunang'ang'ana na kila siku ilivyo. Saa zingine tunasumbuana, saa zingine tunasikizana. Nang'ang'ana tu vile naweza. Bora tu ujue jukumu ni la watu wawili" Alisema Agengo.

Kulingana na Agengo, sio sharti mwanaume awe na uwezo wa kifedha ili awe na uhusiano mzuri na mtoto wake. Alisema kuwa sio sharti mwanaume agharamie mahitaji yote

"Naweza kosa pesa hata miaka 20 lakini haimaanishi ni dhabi. Na haimaaniishi niadhibiwe. Sio eti nadanganya" Agengo alisema.

Alifichua kwamba mama ya mtoto wake wa nne amewahi kutishiwa kuachwa na mpenzi wake wa sasa kwa sababu ya mawasiliano kati yake na mtoto huyo.