"Ningependa kukaa na Bahati nijue jinsi ya kuwa mzazi mwenza" Kabi amezea mate uzazi wenza wa Bahati na Yvette Obura

Muhtasari

•Kabi alisema hali ya kuwa mzazi mwenza ni geni sana kwake kwani ni miezi michache tu ambayo imepita tangu alipogundua Abby ni binti yake•

• Kabi alikiri angependa kushiriki kikao na Bahati ili apate mafunzo kuhusu namna ya kushirikiana vizuri na baby mama katika ulezi wa mtoto.

• Kabi alikiri angependa kushiriki kikao na Bahati ili apate mafunzo kuhusu namna ya kushirikiana vizuri na baby mama katika ulezi wa mtoto.

Image: INSTAGRAM// KABI WAJESUS

Wanavlogu mashuhuri Peter Kabi na Millicent Wambui wa 'The Wajesus Family' wamekiri kwamba wanapendezwa sana na ulezi wenza mzuri uliomo kati ya Bahati na Yvette Obura katika ulezi wa binti yao Mueni Bahati.

Akiwa kwenye mahojiano na SPM Buzz, Kabi alikiri angependa kushiriki kikao na Bahati ili apate mafunzo kuhusu namna ya kushirikiana vizuri na baby mama katika ulezi wa mtoto.

Kabi alisema hali  ya kuwa mzazi mwenza ni geni sana kwake kwani ni miezi michache tu ambayo imepita tangu alipogundua Abby ni binti yake.

"Saa hii natazamia kukaa tu chini na Bahati nijue kuhusu suala la uzazi wenza. Hilo ni jambo geni kwangu kwa sasa. Huwa naona wanaweza kuweka mtoto pale na kufanya mambo mbalimbali. Ningependa kujua mambo kadhaa kutoka kwao" Kabi alisema.

Mke wake Milly Wajesus pia alisema angependa waweze kupata mafunzo kadhaa kutoka kwa familia ya Bahati kwani wameweza kuwa kielelezo bora cha uzazi wenza mzuri.

Alisema pia anapendezwa na bidii yao kazini huku akiwatakia mafanikio zaidi maishani.

Siku chache zilizopita Kabi alifichua kuwa hakuna uhusiano mzuri kati yak na mama ya binti yake ambaye anafahamika kama Shiko.

 Kabi alikiri angependa kushiriki kikao na Bahati ili apate mafunzo kuhusu namna ya kushirikiana vizuri na baby mama katika ulezi wa mtoto.

"Nitaendelea kukazania hilo. Najua sio rahisi kwa hivyo sitarajii ukamilifu. Sitaraji kumuona kila wakati. Saa hii ni ngumu  kumuona lakini nikipata nafasi nitahakikisha tumekuwa na wakati mzuri pamoja"  Kabi alisema akiwa kwenye mahojiano na Mungai Eve.

Amesema anaelewa hali ilivyo kwani hajakuwepo katika maisha ya binti yake kwa miaka saba huku akitumai wakati utafikaambapo hali itakuwa sawa.