Mchekeshaji Akuku Danger ni mgonjwa sana, amelazwa ICU - Sandra Dacha afichua

Muhtasari

•Mwandani wake Sandra Dacha almaarufu kama Silprosa amethibitisha kuhusu ugonjwa mbaya uliomkabili kupitia mtandao wa Instagram.

Akuku Danger
Akuku Danger
Image: Hisani

Mchekeshaji mashuhuri humu nchini almaarufu Akuku Danger amelazwa hospitalini

Mwandani wake Sandra Dacha almaarufu kama Silprosa amethibitisha kuhusu ugonjwa mbaya uliomkabili kupitia mtandao wa Instagram.

 "Babe wangu anaugua sana. Kwa sasa yuko ICU. Maombi yenu yatakuwa ya manufaa sana kwake"  Sandra alisema

Wanamitandao wameeleza wasiwasi wao kuhusiana na habari hizo huku wakionyesha masikitisho yao kuhusu yanayomkumba mcheshi huyo ambaye amekuwa akitumbuiza kwa ubunifu wa kipekee.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za kheri njema ambazo wanamitandao walimwandikia Akuku Danger.

@Mcatricky-ooh,,,pona kakangu Akuku

@lilide16- namtakia apone haraka

@nycewanjeri- itakuwa kheri kwa jina la wmenyezi Mungu 

@sleepydavid - pona haraka kakangu