Akothee afichua anatazamia kuadopt watoto 10, Ashauri wazazi kutotarajia msaada wa watoto wao

Muhtasari

•Kulingana na mwanamuziki huyo, mzazi anaweza kujitolea mhanga kuhakikisha watoto wake wanaishi vizuri ila watoto wale hawawezi kujitolea kusaidia wazazi wao.

Akothee na bnti zake Vesha Okello na Rue Baby
Akothee na bnti zake Vesha Okello na Rue Baby
Image: Instagram

Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu kama Akothee amesema analenga kuasili angalau watoto 10 wa rika tofauti kuanzia 0 hadi miaka 10.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo mwenye umri wa miaka 41 amesema anatazamia kujishughulisha katika kuwa mama pamoja na kuona watoto wa watu wengine wakikua na kufanikiwa mikononi mwake ndiposa akafanya maamuzi yale.

"Ninatazamia kuasili watoto 10 wa rika tofauti, kuanzia umri Sifuri hadi 10 tafadhali 💪 Nataka kushughulika katika kuwa mama na kuona watoto wa watu wengine wakikua na kufanikiwa mikononi mwangu" Akothee amesema.

Kulingana na mwanamuziki huyo, mzazi anaweza kujitolea mhanga kuhakikisha watoto wake wanaishi vizuri ila watoto wale hawawezi kujitolea kusaidia wazazi wao.

Mama huyo wa watoto watano amewashauri wazazi wengine kufuata nyayo zake na kuasili watoto wengi kadri iwezekanavyo huku akiwaeleza kuwa watoto walioasili ndio wataja kuwasaidia baadae.

"Unaweza kujitolea maisha yako yote na anasa kwa ajili ya watoto wako ili waishi maisha bora zaidi, lakini hakuna hata mmoja wa watoto wako anayeweza kujitolea hata wakati wake kwa ajili yako. Jitayarishe kwa jambo hili kama mzazi.  Mama anaweza kulea watoto 7, na saba hao washindwe kutunza mama mmoja tu. Hivyo katika siku yako mapema kabla ya kuzeeka, kufilisika na kuwa mwenye machungu! Chukua watoto wengi uwezavyo, wape sehemu sawa za mali yako kama watoto wako mwenyewe. Utaniambia siku moja, wale walioasiliwa watarudi kukushukuru" Akothee amesema.

Mwanamuziki huyo ana watoto watano, wawili ambao tayari wamehitimu katika chuo kikuu.