"Niliona aibu jamani! Nyota Ndogo asimulia masaibu yaliyompata alipoagiza Ugali kwa kibanda cha Miraa

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo amesema marafiki wake walimcheka sana alipowasimulia yaliyomtendekea  baada ya kila mmoja kukimbia upande wake.

Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Mwanamuziki Mwanaisha Abdalla almaarufu kama Nyota Ndogo amefunguka kuhusu kisa kimoja cha aibu kilichomtendekea hivi majuzi akiwa  jijini Nairobi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nyota Ndogo amesimulia jinsi alivyokuwa anatembea na wenzake kisha mvua kubwa ikaanza kunyesha na kila mmoja akakimbia njia zake ili kutafuta mahali pa kujikinga.

Mwanamuziki huyo kutoka Pwani amesema alipoangalia mbele yake aliona kibanda na kupata afueni moyoni akidhani alikuwa ameangukia mahali pazuri pa kujikinga na mvua. Alikimbia pale na kuingia bila kujua aibu iliyokuwa imemsubiri.

"Nimeketi hapa nimeanza kucheka mwenyewe nimekumbuka nilipokua Nairobi juzi tulikua tunatembea tu na wenzangu kidogo mvua ikaanza kila mtu akakimbia kivyake kujikinga mvua . Mimi niliona Kibanda nikaingia mbio sikutaka kujua nimeingia wapi nikicheki ndani nikaona waume watupu maneno yakanitoka eti naweza kupata ugali samaki jamani Kibanda chakuuza Mira. Waliniuliza umeona mtu akisonga ugali hapa kama unakimbia mvua ngoja vua imalize kunyesha wewe ni nini umeona samaki hapa?" Nyota Ndogo alisimulia.

Mwanamuziki huyo amesema marafiki wake walimcheka sana alipowasimulia yaliyomtendekea  baada ya kila mmoja kukimbia upande wake.