"Nimekuwa na mawazo ya kujitoa uhai" Brendah Johs akiri

Muhtasari

•Afya yangu ya akili imekuwa na changamoto, nimejikuta nikifanya mambo ambayo sikuwa kufikiria ningefanya. Nimejikuta nikilewa kupita kiasa, kula kupita kiasi, kulia sana ...Nimkuwa nikitamani kujiua na nilihisi kama ninataka tu kukomesha kelele kutoka kwa walimwengu maishani mwangu

Brendah Jons
Brendah Jons
Image: Instagram/Brendah jons

Mchekeshaji Brendah Jons amejitokeza wazi na kueleza  mambo magumu ambayo amekuwa akipitia maishani.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Jones ameelezea shinikizo alilopata kutoka kwa mitandao wa kijamii ambalo alitaja kama chanjo cha msongo wa mawazo.

Jones alieleza mambo mengi yamekuwa yakimsumbua na kumshinikiza kutenda vitendo hajawai fikiria angewahi kutenda.

"Hivi majuzi, Afya yangu ya akili imekuwa na changamoto, nimejikuta nikifanya mambo ambayo sikuwai kufikiria ningefanya. Nimejikuta nikilewa kupita kiasa, kula kupita kiasi, kulia sana ...Nimekuwa nikitamani kujiua na nilihisi kama ninataka tu kukomesha kelele kutoka kwa walimwengu maishani mwangu" Alieleza Brendah 

 Aliendelea kusema amekionekana shwari anapoigiza, ila ndani yake kumekuwa na mambo mengi ambayo yamekuwa yakimsumbua. Alitangaza  kuwa amechukua likizo rasmi hadi wakati afya yake ingeboreka.

"Nataka tu uhuru wa kweli na kupumzika... Najua itamkumbusha mtu kuwa ni sawa kutokuwa sawa, na ni sawa kuchukua mapumziko kutoka kwa ulimwengu na kujizingatia mwenyewe ... kwa hivyo ninachukua mapumziko ya afya kutoka kwa kila kitu, ninahitaji tu kukaa kimya na kusikiliza. mwenyewe na kupona. Sijui jinsi gani lakini najua kuwa nina watu wa kweli maishani mwangu" Alisema Brendah.